Wema Sepetu Afunguka Kwanini Anapenda Kuishi na Wanaume Mashoga Nyumbani Kwake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Afunguka Kwanini Anapenda Kuishi na Wanaume Mashoga Nyumbani Kwake

Wema Sepetu amefunguka kuhusu tabia yake ya kufanya urafiki na wanaume tata (mashoga) na ata kuishi nao nyumbani kwake.

Akiongea na Global Publishers, Wema alieleza kuwa anawapenda na anafurahi sana kutangamana na mashoga kwani yeye hana chuki nao kama watu wengine.

“Mimi sijui ni kitu gani lakini ninawapenda sana hao watu na ninafurahi sana kuwa nao maana hata mama alikuwa hapendi kabisa kuona wapo kwangu lakini sasa amewazoea na ninaona nao ni binadamu kama mimi,” Wema Sepetu alisema.

Mrembo huyo pia alifunguka kuhusu nia yake ya kutaka kufunga uzazi atimiapo umri wa 32 (kwa sasa ana 29) iwapo hatakuwa amefanikiwa kupata mtoto.

“Ndiyo na tena safari hii nisipobahatika kupata mtoto hadi ninafikisha umri wa miaka 32 nitafunga kizazi,” Wema Sepetu alieleza.


-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.