Mwana FA: Sijawahi Kumuhonga Mwanamke Pesa Ili Anipende - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwana FA: Sijawahi Kumuhonga Mwanamke Pesa Ili Anipende

RAPA asiyechuja kwenye muziki wa Hip Hop Bongo, Hamis Mwijuma ‘Mwana FA’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa katika maisha yake yote ya ujana, hajawahi kumhonga mwanamke pesa ili apendwe.

Akichonga na Risasi Vibes, Mwana FA alisema tabia ya kuhonga honga wanawake pesa na vitu vingine vya thamani ili kupendwa hilo kwake halijawahi kutokea tangu alipopata akili mpaka alipo sasa kwenye ndoa.

“Nihonge ili nipate nini, sijawahi kuhonga hata siku moja najua wengi wanaweza wasiamini lakini ndiyo hivyo, tabia hizo naishia kuziona kwa washkaji zangu huku mtaani lakini kwangu hazijawahi kuwepo maana kitendo hicho nakichukulia kama biashara ya kikahaba ambayo binafsi naichukia” alisema Mwana FA

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.