Kazi Kubwa Aliyonayo Jux Kwa Sasa ni Kumlinda Vanessa Mdee - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kazi Kubwa Aliyonayo Jux Kwa Sasa ni Kumlinda Vanessa Mdee

Msanii Jux amesema sasa hivi ana kazi kubwa ya kumlinda aliyekuwa mpenzi wake, Vanessa Mdee machoni mwa watu ili asiweze kuonekana mbaya kwa chochote atakachokifanya baada ya kuachana kwao.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Jux amesema Vanessa sasa hivi yupo kwenye wakati mgumu katika kufanya mambo yake ya kawaida, hivyo ni jukumu lake kuhakikisha haeleweki vibaya mbele za watu.

“Kuna vitu mimi siwezi kuvifanya ili kumlinda na yeye hawezi kufanya kunilinda mimi, japo watu watasema vingi hasa kwa mwanamke pale anapoamua kufanya baadhi ya vitu vyake binafsi. Natakiwa kumlinda Vanessa sasa hivi kwa kuwa kila jambo ambalo atalifanya watu watamfikilia vibaya hivyo napaswa kumlinda kutokana na hilo kwa sababu wanawake wenyewe wako wachache”, alisema Jux.

Jux aliendelea kwa kusema kuwa wakati bado wako kwenye mahusiano Vanessa alikuwa na uhuru wa kufanya jambo lolote, kwani karibia kila mmoja aliamini yupo na Jux ndiye mtu wake.
“Muda mwingine anaweza akashindwa hata kufanya vitu vingine, mwanzo hata akionekana na mtu wana-shoot au wanafanya nini, wanajua yupo na Jux, lakini sasa hivi hawezi”, alisema Jux
Pia Jux aliweka wazi kuwa ingawa bado ana kidonda cha maumivu ya kuachana na mpenzi wake huyo, lakini haikuwa ngumu kwao kufikia uamuzi huo, kwani kabla ya kuanza mahusiano walikuwa marafiki wa kawaida, kitu ambacho mpaka sasa bado wanacho.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.