Juma Nature Amtolea Uvivu Gigy Money - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Juma Nature Amtolea Uvivu Gigy Money

Msanii Juma Nature amewakingia kifua wasanii wa kike wa zamani ambao Gigy Money amesema walikuwa hakuna cha maana wanachokiimba, na kumtaka atulie kwani bado ni mdogo kwenye tasnia.

Akizungumza na mwandishi wetu Juma Nature amesema kitu ambacho Gigy Money anatakiwa kufanya sasa hivi ni mazoezi ili aweze kuandika nyimbo, na sio kuongea hovyo kuponda watu wazima, kwani hajapitia mikiki kwenye maisha ya muziki.

"Hawezi kuwa na dharau wakati mtu mwenyewe hata albam saba hajafikisha, bado mdogo sana afanye mazoezi atunge nyimbo zenye hekima, anaweza akapata matuzo kibao, lakini asiongee ongee hovyo bado mdogo sana huyo mtoto, hajawahi kupata mikiki, aingie kwenye mikiki mikiki awaulize wenzake kina Zay B  watamfundisha wanawake wenzake, sisi wanaume kwetu ndiyo asiingie kabisa kwa sababu huku vitani", alisema Juma Nature.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.