Wolper Afunguka Kuhusu Kuwa na Wivu na Harmonize, Pia Kuwa na Mpenzi Mpya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wolper Afunguka Kuhusu Kuwa na Wivu na Harmonize, Pia Kuwa na Mpenzi Mpya.

Mwigizaji staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka na kueleza kuhusu kuwa katika mahusiano na mwanaume mwingine ambaye kwa mujibu wake ni BFF yaani Best Friend Forever ingawa hawako mapenzini.

Kupitia The Weekend Chart Show ya Clouds TV, Wolper amesema hana wivu na mpenzi wake wa zamani Harmonize ambaye kwa sasa yuko mapenzini na mpenzi wa kizungu.

”Tumeachana kama miezi sita hivi tulikuwa hatulewani. Huyu BFF yaani Best Friend Forever tuna kama wiki hivi. Tulikutana vizuri tu alianza kuniona kama miaka minne hivi before. Kinachonivutia kwake ni mpole na mkweli, kwa hiyo ni rafiki yangu mzuri sana"


“Mimi siwezi kuingia kwenye vita na siwezi kuwa na uchungu japo stress hazifichiki na furaha haifichiki. Kwa hiyo nyie mnaweza mkajadili. Vitu vya instagram siyo vya kweli vyote japo wanakuwa na vitu vyao vina ukweli kidogo"

“Huyu kaachana na mtu wake miezi miwili halafu mwezi wa tatu tukakutana. Kwa hiyo, hizo ni story tu wote tumekutana single ila tofautisha wale ni wapenzi na sisi ni BFF na tupo serious. Ni marafiki wa kweli. Mimi siyo mtu wa TV naye siyo mtu wa TV.”
– Jacqueline Wolper.


Diamond Platnumz Akimwimbia Zari Wimbo ENEKA' | LIVE ....Ipo Hapa Chini.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.