Wiz Kid Amchana Davido Asema Ana Sauti Kama ya Chura. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wiz Kid Amchana Davido Asema Ana Sauti Kama ya Chura.

Beef la madogo wawili kutoka kiwanda cha Muziki wa Nigeria linazidi kuwa kubwa kila siku, madogo hawa walikua washkaji baadae zikatoea ishu ambazo zilipelekea kutoelewana. Likaja beef likazimwa kiaina na tukaona wako pamoja wanapiga misele nini, hapa kati tena limeibuka.

Washkaji wamerushiana maneno sana kwenye mitandao ya kijamii wiki chache zilizopita Davido akitumia Snapchat na Wizkid akitumia Twitter.

Utakumbuka kuwa Wizkid alisema Davido ni mtoto mdogo sana na kuwa ni msanii Local, sasa nae Davido kwenye ngoma mpya ya Olamide Summer Body amemjibu Wizkid kwa kumwambia yeye sio msanii Local na kwa kuthibitisha hilo. Davido alisema ana passport ya Marekani kwa hiyo sio msanii local.

Wizkid akaona unisinitanie bwana mdogo, akazama Twitter na kumpaka choo Davido kumwambia Passport ya Marekanu haiwezi kutibu sauti la Chura. 

Tweet ya Wizkid ilikuwa hivi “My people make una remember say Yankee passport no be baba blue, e no dey cure frog voice.” American Passpoer doesnt cure frog voice!

Ni kweli Davido ana sauti la chura ?

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.