Taarifa Kamili Kuhusu Kifo Cha Mtoto Bradley Lowery Shabiki Aliyegusa Nyoyo Za Wengi Duniani. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Taarifa Kamili Kuhusu Kifo Cha Mtoto Bradley Lowery Shabiki Aliyegusa Nyoyo Za Wengi Duniani.


Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia.

Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao kwa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.

Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.
Bradley alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Mei akiwa na Jermain Defoe na Vito Mannone

Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.

Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii.

"Mvulana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo.

"Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake."
Mamake Bradley Gemma Lowery alikuwa awalia mesema mvulana huyo alikuwa amedhoofika sana

Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana.

Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa.

Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".
Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.
Bradley alitawazwa Mtoto wa Ujasiri katika tuzo za Fahari ya Kaskazini Mashariki
Bradley aliipenda sana Sunderland AFC na alikaribishwa uwanjani Stadium of Light
Haki miliki ya pichaPAImage captionMkusanyiko wa picha za Bradley zilizotolewa wakati wa sherehe za siku ya sita ya kuzaliwa ya Bradley mwezi Mei mwaka huu
Mashabiki wa Sunderland walikuwa na bango kubwa uwanjani la kumuunga mkono Bradley wakati wa mechi yao dhidi ya Swansea mwezi Mei
Bradley alitembea kwenye zulia jekundu wakati wa hafla ya Tuzo za Mchezaji Mashuhuri wa Mwaka wa BBC 2016
Bradley na babake Carl mechi kati ya Everton na Sunderland

Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi mwaka jana, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.
Bradley aliunda urafiki na Jermain Defoe

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.