Roma Aweka Wazi Kilicho Mzimba Mdomo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Roma Aweka Wazi Kilicho Mzimba Mdomo.

Roma Mkatoliki amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa zilizomfanya kutokusema nini kilichopelekea yeye kutekwa na nini kilikuwa kinaendelea wakati akiwa chimbo na kudai aliamua kutumia busara ya kutokusema ili mwisho siku aendelee na kazi ya muziki.

Roma Mkatoliki alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza toka alipoonekana kutoka chimbo walipokuwa baada ya kutekwa.

Roma Mkatoliki amesema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema alitambua kuwa anaweza kuwakwaza baadhi ya watu kwa kutokusema na kuweka wazi lakini alifanya maamuzi hayo kwa lengo la kulinda sanaa yake na maisha yake kiujumla.

"Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka ni zaidi ya muziki japo chanzo ni muziki ndiyo maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani, wala nyumbani unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani, wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile tunamaliza pale halafu usiku mwema, lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea,labda ningesema ukweli pengine ungekuwa mwisho wa Roma kwenye muziki, mashabiki wangeshangilia lakini wadau mbalimbali mchongo ndiyo ungekuwa umekwisha"
alisema Roma Mkatoliki

Roma aliendelea kusisitiza kuwa kama angeweka wazi jambo hilo siku ile ambayo ametoka huko chimbo ingepelekea yeye kuacha muziki na kurudi Tanga kufanya mambo mengine kwani hakuna mtu ambaye angetaka kuwa karibu naye tena.

"Hata wewe hapo Dullah usingenipigia simu kunialika kwenye show hapa leo, nakwambia ungeniogopa, na mwisho wa simu Roma angerudi zake Tanga kushika jembe akalime, Je, mashabiki wangependa? Kwanini Roma sasa asiendelee kubaki halafu mashabiki wakaendelea kusikiliza ngoma zake na akaendelea kushusha dude kwa dude, kwa hiyo utaona kuwa yalihitajika maamuzi ya busara katika hili ila nashukuru sana wananchi na wabunge kwa kupaza sauti zenu mpaka tukaweza kutoka na kurudi mtaani kama hivi" alisema Roma Mkatoliki.

Mbali na hilo Roma Mkatoliki anasema toka ametoka mpaka sasa hataki hata kutazama video mbalimbali ambazo zinaonyesha jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kuwatafuta ili waweze kupatikana anadai hataki kutazama sababu hataki kukumbuka kabisa, hali ambayo alikuwa nayo kipindi hicho huku akisema hapendi kuona mtu mwingine yoyote anakwenda huko chimbo ambako wao walikuwa wamewekwa wakipata mateso hayo.

Mwanzoni wa mwezi wa 4 mwaka huu msanii Roma Mkatoliki, Moni Cetrozone, Binladen na Emmanuel walitekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe Records na kukaa kusikojulikana kwa siku tatu na baadaye kuja kuonekana wakiwa na majeraha mbalimbali.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.