Peter Msechu: Nakubali Kukosolewa Lakini Sio Kuhusu Tumbo Langu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Peter Msechu: Nakubali Kukosolewa Lakini Sio Kuhusu Tumbo Langu.

Msanii wa Bongo Flava, Peter Msechu amesema si kweli huwa anachukia akikoselewa kama wimbo wake haujafika kiwango stahiki.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Pakawa’, ameiambia Ladha 3600 ya E Fm kuwa asichokipenda ni ukosoaji wa mitandaoni usiofaa ambapo hivi karibuni alimcharukia vikali kijana mmoja aliyekosoa ngoma yake.

“Yule dogo ameshakosoa vitu vingi, nilimpost mwanangu akasema ana upele, kuna siku nilipost chakula akasema kimezidi chumvi, yule dogo ananifuata sana lakini sitoki povu naamni kazi zangu ni kubwa na kimsingi muendelezo umekuwa ni ule ule, Yakawa ni muendelezo wa Malava,” amesema na kuongeza.

“Nakubali kukosolewa kwa sababu ningekuwa na mia, kwa sababu nilikubali kurekebishika kwenye Nyota kwa kuandikiwa ndio maana hadi leo nimetoboa, kwa hiyo nakubali kukosolewa lakini habari za tumbo langu mziache,” amemaliza kwa kusema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.