Jack Wolper na Skendo ya Kupora Mume wa Mtu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jack Wolper na Skendo ya Kupora Mume wa Mtu.


SAKATA la staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper kudaiwa kupora mume wa mtu aliyefahamika kwa jina moja la Brown, mwenyewe amecharuka kwa kutamka kwamba kama kuna mtu anasema huyo ni mumewe basi ajitokeze hadharani kuliko kusemamitandaoni.

Akizungumza na Amani, Wolper alisema wakati hayupo na Brown, hakuna mtu aliyeibuka na kusema huyo ni mumewe, lakini tangu aanzishe naye uhusiano, miruzi imekuwa mingi ya wanawake kuibuka kila kukicha wakidai mume wao.

“Kinachonishangaza ni kitendo cha mimi kuwa naye tu ndiyo watu wanaanza kuibuka na kusema eti ana mke, duh!

“Mbona kipindi siko naye, hakuna mwanamke ambaye alikuwa anasema ni mumewe. Sasa basi kama kuna mwanamke ambaye anadai ni mumewe ajitokeza hadharani.

“Nilichogundua baadhi ya wanaoibuka ni wale ambao waliwahi kuwa naye kitambo, sasa nasema hivi, huyo anayesema ni mume wake basi ajitokeze,” alisema Wolper.
Amani lilimsaka pia mwanaume huyo ambaye anadaiwa ku-date na Wolper, Brown ambaye baada ya kusomewa madai yake alisema hana mwanamke mwingine ambaye yuko naye kwenye uhusiano zaidi ya Wolper na kudai mwanamke aliyeibuka ni exwake.

“Sina mwanamke mwingine niliyenaye kwenye uhusiano zaidi ya huyo unayemjua, ninachojua ni kwamba mwanamke aliyeibuka na kudai mimi ni mumewe huyo ni ex wangu ambaye tuliachana kitambo sana hata wakati sijawa na uhusiano na mwanamke niliyenaye sasa.

“Kitu cha kujiuliza, alikuwa wapi siku zote jamani kama siyo kuniharibia?” alihoji Brown.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.