Jack Wolper Aweweseka Juu ya Mpenzi Wake Mpya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jack Wolper Aweweseka Juu ya Mpenzi Wake Mpya.


KWA kuonyesha ni kumpa dongo mpenzi wake wa zamani, staa mwenye mvuto wa kipekee Bongo Muvi, Jacqueline Wolper amesema kuwa katu hawezi kumuweka hadharani mpenzi wake mpya kwa kuogopa kuibiwa tena na wazungu.

Staa huyo alituma dongo hilo kupitia mtandao wake wa Snapchat, ambapo alikuwa akisema kuwa, anatamani sana kumuweka hadharani mpenzi wake huyo mpya lakini anaogopa kunyakuliwa tena na wakware wa kizungu kama alivyofanyiwa kwa mpenzi wake aliyepita ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.

Star Mix hili lilimtafuta Wolper ambaye baada ya kubanwa kutaka kujua jina la bwana huyo aliyenaye alianza kwa kuangua kicheko na kusema kuwa kuna wakati mwingine mtu anazungumza kufurahisha watu wacheke lakini si kwamba kuna mtu kweli kwa sasa.

“Jamani kuna kipindi mtu unawafanya watu wafurahi na kucheka sio kila unachozungumza mtu kiwe cha kweli.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.