Huu Ndio Mchango Wa A.Y Katika Muziki wa Bongo Flava. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Huu Ndio Mchango Wa A.Y Katika Muziki wa Bongo Flava.

Ikiwa leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa kwake, msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yessay A.Y ametajwa kuwa moja ya mtu mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini.

Hayo yamebainishwa na mtangazajiwa kipindi cha The Playlist, Lil Ommy. Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika,”Ulichangia sana kuutangaza muziki nje ya mipaka ya Tanzania na kufungua njia kwa wasanii wengi waliokuwepo na waliokuja baadae. Ulifungua Collabo ya ndani ya Afrika Mahariki na nje ya mipaka yake. Uwekezaji kwenye VIDEOS bora na directors nje ya nchi na kuchallenge industry ya ndani kupata product bora was the great move.”

Ameongeza “Kama ulikuwa hujui AY kila mara alipokuwa akisafiri kwenda nje ya nchi mbalimbali alikuwa anabeba CDs za nyimbo za wasanii wenzake wa Bongo Fleva ambazo ngoma sio hata zake au washkaji zake bila kujali wenyewe wanajua au hawajui na alikuwa akizisambaza katika nchi hizo ili kusambaza zaidi MUZIKI nchini kwao, ili saidia sana kusambaza muziki kipindi hicho mambo ya kudownload na kutuma kwenye mitandao hawakuwa kama ilivyo leo.”

Ameendelea kuongeza, “Kitu kizuri kikubwa alichokifanya siku zote kwenye shows zake nje ya nchi au kwenye Safari zake, hakusita kujigamba kuwa Mtanzania na kujivunia nchi anayotoka. Kumbuka show yake kwenye Big Brother Africa. AY ametoa connections nyingi sana za Collabo, Directors wa VIDEOS kwa wasanii wenzake na mambo mengi ikiwa ushauri etc.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.