Flora Mbasha na Mumewe wa Zamani Waliamsha Bifu Upya, Ipo Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Flora Mbasha na Mumewe wa Zamani Waliamsha Bifu Upya, Ipo Hapa

Waimba Injili Bongo ambao walikuwa wanandoa kabla ya kutalikiana mahakamani, Flora Daud Kusekwa ‘Madam Flora’, zamani alikuwa akitambulika kama Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha wameonekana kuliamsha dude la bifu lao upyaa, Ijumaa Wikienda linakupa mkanda kamili.

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kwa sharti la kutotajwa gazetini, chanzo makini cha sakata hilo kilielezwa kuwa, wawili hao kwa sasa wameingia kwenye bifu upya baada ya hivi karibuni Flora kudaiwa kumtolea maneno (hayaandikiki gazetini wala mitandaoni) aliyekuwa mumewe, Mbasha ambayo yalisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua gumzo.

“Yaani mambo siyo mambo kwani Flora na Mbasha kwa sasa bifu limeanza upya kama zamani wakati wanaachana baada ya mwanamama huyo kudaiwa kutoa maneno mabaya ambayo yalimuudhi Mbasha naye kuamua kufunguka kwenye vyombo vya habari.

“Kwenye habari hiyo mitandaoni ilionesha Flora alizungumza maneno hayo yanayosemekana yamo kwenye kitabu chake ambacho kimeshatoka kinachoitwa Siri za Flora Mbasha, maneno ambayo alisema ndiyo chanzo cha ndoa yake kuvunjika.

“Inasemekana aliwaita watu kupata ufafanuzi zaidi kwenye kitabu chake licha ya kwamba Flora baada ya habari kusambaa mitandaoni alikanusha kuwa hakuwahi kusema maneno yale,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata habari hiyo kutoka kwa chanzo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mbasha ambaye alionekana kuwa mwenye hasira kali akisema:

“Sipendi ujinga kwani watu hawawezi kuuza hicho kidaftari chao mpaka watafute kiki kwangu? Mbona wengine wanauza vyao kwa utaratibu mzuri?

“Mimi ninaingiaje kwenye ishu za huyo Flora? Zaidi ya miaka mitatu sipo naye na ni mke wa mtu, ninamuomba atulie na akome kunitajataja.”

Kwa upande wa Flora alipotafutwa ili kujibu hayo aliendelea kusisitiza kuwa habari hizo za mtandaoni hazikuwa za kweli isipokuwa ni kweli kitabu chake hicho kimeshatoka na kinaelezea kiundani mambo aliyoyapitia kwenye ndoa yake na Mbasha kabla ya kuolewa na David Kusekwa.


GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.