Esha Buhet Afunguka Kuteswa na Mimba Yake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Esha Buhet Afunguka Kuteswa na Mimba Yake

STAA wa sinema za Kibongo, Esha Buhet amefunguka namna anavyoteswa na kisirani cha mimba hivyo kuwaomba watu wamsamehe pindi atakapowakwaza.

Akizungumza na 3-Tamu, Esha alisema kuwa mimba aliyonayo inampa kisirani hivyo inawezekana akawa anawaudhi baadhi ya marafiki na ndugu zake, lakini ni vyema wakaelewa hali aliyonayo kuwa ni ya mpito hivyo wamsamehe.

“Hali niliyonayo ni ya mpito na huwa inakuja na mambo mengi, hivyo ndugu zangu na jamaa zangu nawaomba wanisamehe sana kama ikitokea nikawaudhi maana naona mimba inanipeleka puta,” alisema Esha.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.