Baby Madaha: Wanaume Wana Hali Ngumu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baby Madaha: Wanaume Wana Hali Ngumu

Msanii wa Bongo Flava na Muigizaji wa filamu, Baby Madaha amedai kuwa wasanii wa kiume wana changamoto kubwa ya kufanya vizuri katika muziki ukilinganisha na wasanii wa kike.

Muimbaji huyo amesema kutokana na hilo ni vema wasanii wakawekeza katika vitu vingine ili kuweza kuendesha maisha na kuonya kuwa hata ugumu huo unaweza kuwakumba wasanii wa kike.

“Genderi issue ina base sana kwenye wanawake, wanaume wana hali ngumu kwenye kupita, yaani hiyo tuseme tu ukweli, ukimuona mdogo wako anaingia kwenye sanaa mwambie mwanangu ebu soma kwanza ile ifanye kama support,” ameiambia Daladala Beats ya Magic Fm na kuongeza.

“The same Mama yangu aliniambia soma kwanza ukishamaliza degree yako ndio uingie kwenye muziki, nilipomaliza nikawa nafanya music lakini nina cheti changu. Sasa kwa maisha ya Magufuli unadhani utaishi kwa kutengemea cheti pekee yake, kuna wanamuziki wamegeuka Mama Lishe, wanauza karanga ni kwa sababu wanajua hawatakuwepo pale miaka 50 baadae,” amesisitiza.

Kutoka na hilo amesema ndio sababu ya yeye kufanya biashara zake nje ya nchi (Dubai), pia anajivunia elimu yake kwani anaweza kuajiriwa sehemu yoyote kutokana na cheti chake hivyo hawezi kuishi kwa kutengemea muziki.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.