Wema Sepetu Kusomewa Kisomo cha Kufa Mtu. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wema Sepetu Kusomewa Kisomo cha Kufa Mtu.

DAR ES SALAAM: Kufuatia mabalaa mbalimbali ambayo yamekuwa yakimuandama Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amejipanga kumsomea kisomo maalum ndani ya Mwezi Mtukufu ili kumuepushia yale yote ya shari.

Shehe Mkuu amefikia hatua hiyo kufuatia mdada huyo ndani ya kipindi kifupi kuandamwa na majanga ambayo yamekuwa yakimkosesha amani. Miongoni mwa mabalaa ambayo yememkumba Wema siku za hivi karibuni ni pamoja na lile la kutajwa kwenye listi ya mastaa wa madawa ya kulevya na hili la juzi la kutengenezewa sauti akiongea kimahaba na kiongozi wake, Freeman Mbowe.

Akizungunza na Amani juzi, shehe huyo alisema kuwa, amepanga kumfanya kisomo hicho ndani ya mwezi huu endapo Wema na mama yake watafika katika ofisi zake zilizopo Lumumba jijini hapa kwa maelezo zaidi.

MSIKIE SHEHE MKUU

“Unajua Wema amekuwa akikutana na misukosuko mingi, ninachoweza kusema iwe kweli au si kweli Wema anatakiwa kufanyiwa kisomo maalum. Maana kumbukumbu zinaonesha hapitwi na mabaya mara kwa mara, kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu amuepushie, kisomo nitakiandaa mimi mwenyewe. “Kuhusu sehemu na siku ya kufanya kisomo hicho bado haijafahamika kwa sababu hadi Wema na mama yake watakapokuja na kupanga nami kama ni nyumbani kwao lakini ni vyema wakaja ofisini kwangu. Ninafikiria kisomo hiki kukifanya

ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani,” alisema Shehe Mkuu. Baada ya kumsikia shehe huyo, gazeti hili lilimtafuta Wema na mama yake ili kusikia wana lipi la kusema kuhusiana na uamuzi huo wa heri wa kiongozi huyo wa dini lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kupatikana. Hata hivyo, kwa kuwa ni jambo jema, gazeti hili linamshauri staa huyo kumtafuta Shehe Alhad ili kufanyiwa kisomo hicho kinachoweza kumuepusha na mabalaa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.