Upande wa Alikiba Hawataki Kuwa Karibu na Mimi – Dully Sykes - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Upande wa Alikiba Hawataki Kuwa Karibu na Mimi – Dully Sykes


Msanii wa muziki, Prince Dully Sykes amedai kuwa upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu naye ila upande wa Diamond wanamuonyesha upendo ndiyo maana yupo karibu nao.

Dully amesema kuwa “Upande wa Alikiba hawataki kuwa karibu na mimi ila upande wa Diamond wapo karibu na mimi, sababu hao wapo karibu na mimi na wao wananionyesha upendo ndio maana nipo karibu nao na sina tatizo na AliKiba wala Diamond,”

Dully alisema hayo wakati wa mahojiano na kipindi cha 180 Power cha Sibuka Fm, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho Byno, kuwa baada ya kufanya kazi na Harmonize, watu wanahisi unaupendeleo na upande huo na umeuacha upande mwingine ambao ni Alikiba.

Hits maker huyo wa ‘Yono’ pia alifunguka juu ugomvi wa Diamond na Alikiba na kusema kuwa yeye hawezi kujiingiza katika hilo, yeye ni mtu mzima na ugomvi wao ni wakitoto.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.