Snura 'Sinywi Pombe Wala Sivuti Ili Kuondoa Aibu' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Snura 'Sinywi Pombe Wala Sivuti Ili Kuondoa Aibu'

Msanii wa Bongo Fleva, Snura amedai yeye hatumii kilevi chochote akiwa jukwaani kwa ajili ya kuondoa aibu.

Muimbaji huyo amesema watu wamekuwa wakidhani kuwa anatumia kilevi kabla ya kupanda jukwani kwa namna ambavyo anawafurahisha mashibiki.

“Mimi napanda kwenye stage situmii kinywaji cha aina yoyote Mungu wangu aliyekamili ni shahidi. Sinywi pombe, sivuti na ninapanda kwenye stage ninahamsha kiasi kwamba unaweza kuhisi kuna kitu nimetumia kichwani, akili yangu nimeijenga hii ni kazi, huwezi kuona aibu kwa sababu ndio kazi uliyoichagua,” ameimbia E-Newz ya EATV.

“Kwa hiyo napenda nipande kwenye stage nikiwa mzima timamu nione kwa sababu hii ni kazi yangu naifanya, pia nafanya research kujua style gani nikicheza watu wananishangilia, wimbo gani nikiimba watu wanapenda,” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.