Mbowe Aikana Sauti Inayosambaa Mitandaoni Ikidai Wema Sepetu ni Mpenzi Wake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mbowe Aikana Sauti Inayosambaa Mitandaoni Ikidai Wema Sepetu ni Mpenzi Wake

Habari inayotikisa mitandao ya kijamii kwa sasa ni ile Audio (voice note/Sauti) inayodaiwa kuwa ya Muigazaji Wema Sepetu na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe inayoashiria kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.

Leo kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM Mbowe ameielezea sauti hiyo akisema taarifa hizo anazichukulia kama majitaka:

“Mimi nalichukulia kama taarifa za kawaida za maji taka zinasambazwa. Taarifa ambazo zinatengenezwa hazina ukweli wowote ndio kitu ninachoweza kusema kwa sababu siyo za kweli.

“Timu yangu ya mitandao inajaribu kufuatilia kuhusu kundi ambalo limetengeneza kutuchafua kwani tupo kwenye msiba, kwenye maombolezo na ukweli utajulikana tu muda sio mrefu.

"Sauti siyo ya kwangu. Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana ni mwanachama wetu na kwamba, kama kuna mahusiano sio kweli, ni taarifa za upotoshaji tu."

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.