Masikini Johari wa Bongo Movies, Apata Piga la Maisha ! - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Masikini Johari wa Bongo Movies, Apata Piga la Maisha !


Pole! Staa wa kitambo wa sinema za Kibongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ amepata pigo ‘hevi’ baada ya kufiwa na shangazi yake aliyemlea tangu akiwa mtoto, kumsomesha na kumfundisha maisha hivyo kuondoka kwake kumemuachia maumivu na pigo kubwa.

Johari, akiwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga kuhudhuria msiba huo aliliambia Wikienda kwa njia ya simu kuwa, aliumia mno alipopata taarifa za kifo cha shangazi yake huyo aliyekuwa nguzo muhimu maishani mwake.

“Nimekuja Shinyanga kumzika shangazi yangu, tumeshamzika, lakini kwa kweli ameniacha mpweke sana maana ndiye aliyenilea, kunisomesha na kunifundisha maisha, kiukweli ni pigo kwangu,” alisema Johari.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.