Huu ni Zaidi ya Ukarimu Kutoka Kwa Vodacom Tanzania Foundation
Kampeni ya Ukarimu wa
Vodacom imendeelea kuwafikia watanzania maeneo mbalimbali nchini Tanzania na
kuwafuturisha katika mfungo huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo kampeni
hiyo ina lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa
Ramadhan na katika maisha ya kila siku.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya
sekondari Marwa iliyoko Mikindani Mtwara wakijiandaa kupata futari mwishoni mwa
juma. Vodacom pia wamekuwa wakitangaza maeneo ambayo yatafuatia kuturishwa
katika muendelezo wa kampeni ya Ukarimu.
Watoto wanaolelewa katika kituo
cha kulea yatima cha Mwinyi
Baraka cha Misugusugu Kibaha mkoani Pwani,
wakimsikiliza Glori Mtui ambaye ni mfanya kazi wa Vodacom Tanzania PLC
wakati wakati wa futari iliyoandalia na
Vodacom Tanzania Foundation kwa watoto hao kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu
wa Ramadhani.
Huduma hii pia ina lengo la kuendeleza mshikamano
inawawezesha Waislamu na Watanzania kwa ujumla kujiunga na kifurushi
kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati
wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo
inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na
huduma hii mteja anapiga *149*01#
kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando
linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.
Download App Yetu MPYA >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !
No comments
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.