Zari amtembelea Ivan hospital kumjulia hali - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zari amtembelea Ivan hospital kumjulia hali

Mama watoto wa Diamond, Zari the Bosslady ameonekana katika picha akimjulia hali ex wake Ivan Ssemwanga ambaye anadaiwa kulazwa katika hospital moja nchini Afrika Kusini baada ya kupata matatizo ya moyo.
Ivan ambaye alipata watoto watatu na Zari, anadaiwa kukimbizwa hospital wiki hii baada ya kupoteza fahamu.

Jumatatu hii Zari alipost picha ya mshumaha na kuwaomba mashabiki wake kumuombea mzazi mwenzake huyo.

Hapo jana Zari kupitia ukurasa wake wa SnapChat aliandika “Siku mbili kwangu zimekuwa ngumu, nawaomba tumuombee Ivan”.

Mitandao ya Uganda inadai kuwa Ivan anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.