Young Dee: Sina Mahusiano na Amber Lulu, Me Niko Single - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Young Dee: Sina Mahusiano na Amber Lulu, Me Niko Single

Siku za hivi karibuni kumeonekana kuwa na ukaribu baina ya msanii Young Dee na video vixen Amber Lulu, wawili ambao hapo awali ilisemekana kuwa waliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na baadaye kusemekana kuwa mrembo Tunda alichukua nafasi ya Amber Lulu kwa Young Dee.Amber Lulu na Young Dee kwenye Bongo Bahati Mbaya

Ukaribu wa Young Dee na Amber Lulu umezua maswali mengi kwa wengi na kuhisi kuwa wawili hao wamerudiana tena katika mapenzi, kitu ambacho Young Dee amekanusha.

Akiongea na Clouds E ya Clouds TV, Young Dee amefunguka kuwa hana ukaribu wowote na Amber Lulu ila tu sometimes huwa wanakutana kwa bahati mbaya.

“Tumekutana tu kwenye project yangu ya Bongo Bahati Mbaya, kwasababu naye pia ni msanii sometimes tunakutana tu bahati mbaya. Ila mimi niko single ninachoweza kusema ni kuwa nina mtoto wa kike anayeitwa Tamal bas.” Alisema Young Dee.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.