Wananchi wapewa tahadhari na Tanesco - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wananchi wapewa tahadhari na Tanesco

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa tahadhari kwa wananchi likiwataka wasikae wala kufanya shughuli zozote karibu na miundombinu yake kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchi nzima.

Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco nchini, Dk Tito Mwinuka amesema miundombinu ya umeme nchini kwa sasa inapata hitilafu za mara kwa mara hivyo wananchi wachukue tahadhari.

Dk Mwinuka amewataka wananchi kutoa taarifa mapema inapotokea hitilafu yoyote kwenye miundombinu ya umeme wakati mvua zinapoendelea kunyesha.

"Wasikae chini ya transfoma ya umeme… tunawaomba wananchi kutoa taarifa mapema maeneo yenye mafuriko au mkusanyiko wa maji mengi ili kusaidia kuchukua tahadhari," amesema Dk Mwinuka.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.