Wachezaji hawa wa Yanga wafungiwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wachezaji hawa wa Yanga wafungiwa

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni 5 kwa makosa mbalimbali yaliobainika kuyafanya kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa ligi kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika wa 2016/17.

Kamati ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni kuhusiana na wachezaji wa timu hiyo kumuangusha mwamuzi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC na imewamua kuwasimamisha kuitumikia Ligi Kuu Bara.

Wachezaji hao ni Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu wakati wakisubiri suala lao la kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mwamuzi Ludovic Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi yake ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.