Taarifa Mpya kutoka Mamlaka ya hali ya hewa, Dar imetajwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Taarifa Mpya kutoka Mamlaka ya hali ya hewa, Dar imetajwa

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), imesema hali ya vipindi vifupi vya mvua katika maeneo ya mwambao wa pwani ya Kaskazini itaendelea hadi Mei 9.

Taarifa ya tahadhari iliyotolewa na TMA leo saa tisa alasiri inasema kunatarajiwa kuwapo vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24. Mamlaka hiyo imesema maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani. Pia, visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imesema hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini.

“Wakazi wa maeneo tajwa wanashauriwa kuchukua tahadhari na hatua stahiki. Mamlaka inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo kila itakapobidi,” imesema taarifa ya TMA.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.