Snura sasa afikiria ndoa na watoto - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Snura sasa afikiria ndoa na watoto

Mwanamuziki na Muigizaji, Snura Mushi amefunguka na kusema anatamani kumpatia mwanaume atakaye funga naye ndoa watoto wawili ili kukamilisha idadi ya watoto wanne ambao ni ndoto ya kuwapata.

Snura amefunguka hayo katika kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa radio, 'Personality of the Week', na kusema kuwa pamoja na kwamba tayari ameshapata watoto wawili ambo wamepatikana kinyume cha sheria za dini bado anatamani kuongeza wengine wawili akiwa ndani ya ndoa.

"Sijafikia mwisho wa kuzaa kwani nina ndoto ya kuwa na watoto wanne, tayari hapa nilipo nina watoto wawili  lakini sijawapata kwa njia sahihi kufuata sheria za dini kwa maana nimewapata nje ya ndoa. Nikipata mume nikafunga naye ndoa ndio nimzawadia watoto wawili kama zawadi ya kufunga ndoa na mimi na hapo nitakuwa nimeshatimiza idadi ya watoto wa nne"- Snura alifunguka.

Akifunguka kuhusu wazazi wenzie Snura ameelezea jinsi alivyopata bahati mbaya ya kukataliwa na wanaume wawili ambao amezaa nao

"Wazazi wenzangu walikataa mimba zikiwa changa, mtoto wangu wa kwanza alikataliwa na baba yake tangu nikiwa na ujauzito wa wiki mbili na huyu wa pili baba yake alimkana akiwa na mwezi mmoja hivyo sijawa na bahati ya watoto wangu kukubaliwa na baba zao lakini hawajawahi kuwa na manung'uniko ya kusema kwa nini sisi hatuna baba kwa sababu mapenzi ninayowapaia wanaridhika nayo"- Snura aliongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.