Siwezi Kumshauri Magufuli - Jay Moe - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siwezi Kumshauri Magufuli - Jay Moe

Rapa Jay Moe anasema kama akipata nafasi ya kukutana na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli hataweza kumshauri jambo lolote kwa kuwa yule ni Rais wa nchi bali yeye atamuomba awafikirie wasanii na kuona umuhimu wao.

Jay Moe amesema hayo na kusisitiza wasanii walikuwa na mchango mkubwa katika uchaguzi uliopita ambao umesaidia viongozi wengi kuingia madarakani
"Nitamuomba Magufuli maana siwezi kumshauri yule ni Mh. Rais wa nchi bali nitamuomba atufikirie na aone umuhimu wetu, kwa sababu mchango wetu umetumika sana katika uchaguzi uliopita, tumeweza kwenda 'endorse' kuithinisha wagombea na vitu kama hivyo kwa hiyo waone kwamba imefika muda na wao kutoa shukrani kwa kile ambacho sisi tulikifanya kwa kufanikiwa kwao kushinda, matatizo yetu sisi wasanii yanajulikana tuna mfumo mbovu sana wa masoko, mzuki wetu mzuri lakini haujulikani utauzwa wapi nadhani kupitia serikali na idara zake kama COSOTA, BASATA, Waziri wanaweza wakakomaa wakaweka nguvu fulani" alisema Jay Moe  

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.