Simon Msuva ashonwa nyuzi nne - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simon Msuva ashonwa nyuzi nne

Simon Msuva ambaye jana aliipatia Yanga goli la kwanza katika dakika ya saba ya mchezo wakati klabu hiyo ikicheza na Mbeya City, Msuva aliumia na kupelekea kutoka mchezoni dakika za kwanza baada ya kugongana na mchezaji wa Mbeya City wakati akifunga.

Kwa mujibu wa taarifa ya daktari wa Yanga inasema kuwa mchezaji huyo ameumia sehemu ya juu ya uso wake baada ya kuchanika na kushonwa nyuzi nne.

"Saimon Msuva amechanika juu ya jicho lake la kushoto ambapo ameshonwa nyuzi nne baada ya kugongana na mchezaji wa Mbeya city wakati akifunga goli lake la 14 kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu" Yanga

Simoni Msuva mpaka sasa anaongoza kwa ufungaji katika Ligi Kuu Tanzania bara akiwa na magoli 14 akifuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting wote wakiwa na magoli 12.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.