Simba: Kufa kupona dhidi Mbao fainali FA - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Simba: Kufa kupona dhidi Mbao fainali FA

KIPA CHAGUO LA KWANZA WA SIMBA, DANIEL AGYEI.

KIPA chaguo la kwanza wa Simba, Daniel Agyei, amesema hawahofii Mbao FC, lakini mechi dhidi yao itakuwa ngumu kwa sababu kila timu inahitaji kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani, hivyo watapambana mwanzo mwisho kuhakikisha wanashinda.

Mbao FC ya jijini Mwanza itakutana na Simba katika fainali ya mashindano ya Kombe la FA itakayopigwa Mei 27, mwaka huu baada ya juzi kuwavua ubingwa Yanga kwa kuwafunga bao 1-0.

Akizungumza na gazeti hili jana, Agyei alisema mechi hiyo itakuwa na ushindani na ili waweze kusonga mbele watatakiwa kupambana hadi dakika ya mwisho.

Agyei aliongeza kuwa katika kikosi cha Simba wachezaji wote wanajua jukumu linalowakabili na wameahidi kupambana ili kuwafurahisha mashabiki na wanachama wa timu hiyo na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

"Mbao ni timu nzuri, si ya kuibeza, tunatakiwa kucheza katika kiwango chetu ili kupata ushindi, tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda katika mechi hiyo muhimu, tulikuwa tunasaka kufika fainali, kinachofuata ni kushinda mchezo wa fainali," alisema kipa huyo wa zamani Medeama FC ya Ghana.

Aliongeza kuwa mbali na mchezo huo wa Kombe la FA, pia wanataka kupambana pia kushinda mechi tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizobakia dhidi ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam, Mwadui FC na Stand United zote kutoka Shinyanga.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.