SHILOLE ASEMA HAMKUBALI KABISA ALI KIBA ILA ANAMKUBALI DIAMOND - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

SHILOLE ASEMA HAMKUBALI KABISA ALI KIBA ILA ANAMKUBALI DIAMOND

Zuwena Muhamed alimaarufu kama 'Shilole, amesema yeye hamkubali msanii Alikiba na hana sababu ya kutomkubali na ila yeye anamkubali zaidi Diamond Platnumz .
.
.
Shilole amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI live kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane kamili mpaka saa kumi jioni. "Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Alikiba, nampenda Diamond kutoka na mambo yake na vile alivyo, kwa hiyo kila mtu ana watu anaowakubali na kuwapenda" alisema Shilole
Mbali na hilo Shilole anasema yeye alishtuka mapema na kuchomoka kwenye tasnia ya bongo movie maana kama aliona kuwa mbele itakuja kuwa tia maji tia maji na kusema saizi yeye ameridhika na muziki kwani muziki unamlipa na umempa mafanikio makubwa ambayo kama angekuwa kwenye filamu huenda asingepata.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.