Ronaldo avunja rekodi awa mchezaji wa kwanza kuwa na wafuasi 100m Instagram - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ronaldo avunja rekodi awa mchezaji wa kwanza kuwa na wafuasi 100m Instagram

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji soka wa kwanza duniani kuwa na wafuasi 100 milioni katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Aliandika historia nyingine wiki hii, baada ya kufunga hat-trick yake ya 47 katika uchezaji wake wa soka ya kulipwa.

Mchezaji huyo kutoka Ureno pia ana mashabiki wengi zaidi kwenye Instram kuliko mwanamume mwingine yeyote yule. Ndiye wa sita katika kufuatwa na watu wengi zaidi mtandao huo duniani.

Wanaomzidi pekee ni Beyonce, Taylor Swift, Ariana Grande, Selena Gomez na akaunti yenyewe ya Instagram.

Ronaldo ana wafuasi wengi kuwashinda Kim Kardashian, Jenner, Justin Bieber na Dwayne ‘The Rock’ Johnson.
Katika soka, anayemfuata ni nyota wa Barcelona Neymar aliye na wafuasi 74m.

Lionel Messi anakaribia kutimiza wafuasi 71m, David Beckham ana 36m na James Rodriguez ana 30m.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.