ROMA: Kamwe Sina Nidhamu ya Uoga. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

ROMA: Kamwe Sina Nidhamu ya Uoga.

Staa asiyechuja wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa katika maisha yake ya kimuziki, hajawahi kuwa na nidhamu ya uoga kama ambavyo baadhi ya watu wanavyomponda.

Roma alifunguka hayo wikiendi iliyopita alipokuwa akipiga stori na Uwazi Showbiz kufuatia maneno kutoka kwa mashabiki wake kuwa muziki wake utachenji kutokana na hofu, tofauti na alivyozoeleka kuwa na mashairi makali ya kuikosoa serikali.

“Kamwe sijawahi kuwa na nidhamu ya uoga maishani mwangu, kinachotokea kwa sasa ni mabadiliko tu ya muziki wangu, siwezi kuimba siasa kila siku, ukweli ni kwamba kwa kuimba siasa kila siku zinafanya muziki wangu usiwe wa kimataifa na uwe ni muziki wa ndani,” alifunguka Roma ambaye bado hajapona makovu aliyoyapata.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.