Rayvanny afunguka haya kuhusu Sugu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Rayvanny afunguka haya kuhusu Sugu

Rayvanny

Msanii Rayvanny amesema Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ni mtu ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa katika video yake ya ‘Zezeta’.

Rayvanny amesema Sugu ndiye alimpa idea ya video hiyo mara baada ya kumtumia wimbo, ndipo alipomshirikisha na director Erick Mzava na kuanza kushoot.

“Ni mtu poa sana, ni mtu ambaye alijiweka mbele kwenye suala la kijana wake, ninakumbuka hata tulipoenda kushoot mambo ya location yeye ndiye alikuwa anapangilia utafikiri video yake.

“Ni mtu ambaye ananirespect ingawa kanipita sana mimi umri na nyadhifa. Nimepata tatizo niko Mbeya, kuna matatizo yalitokea na Polisi nikampigia simu mara moja tu tukasuluhisha, kwa hiyo ni mtu ambaye anajitoa sana kwetu, so wasanii wengine ambao wanatokea Mbeya waige mfano ,” Rayvanny alikiambia kipindi cha XXL.

Kuhusu baadhi ya wasanii wa Mbeya kukosa ushirikiano katika muziki, Rayvanny amesema, “Mimi nafikiri kwa sababu tu hatuja link pamoja, alafu kitu kingine suala la chuki naweza kusema, tumejitengenezea mazingira ya kuvimba, achana nae, yeye nani?, hii siyo nzuri kikubwa tuwe na umoja tusaidiane wenyewe hata wale wasanii wachanga wa Mbeya tunaweza tukawashika mkono,” alimaliza kwa kusema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.