Ray C - Naliaga Nikiambiwa Wimbo Wangu Mbaya. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ray C - Naliaga Nikiambiwa Wimbo Wangu Mbaya.

Msanii mkongwe anayetamba kwa sasa na wimbo wa 'Unanimaliza', Rehema Chalamila ' Ray C' amefunguka kuwa machozi huwa yanamdondoka pindi anapomsikilizisha mtu wimbo ambao anaamini utafanya vizuri alafu akajibiwa hautokuwa 'hit'.

Ray C amefunguka hayo leo kwenye Planet Bongo wakati akitambulisha wimbo wake mpya na kueleza kuwa kabla hajapeleka wimbo kwenye Radio huwa anasikilizisha watu na anapopata majibu tofauti na alivyofikiria huwa yanamuumiza na kumfanya atengeneze ngoma nyingine kali akiwa na machozi.

"Kabla sijatoa wimbo nina tabia ya kuwasikilizisha watu wa chache ambao naamini wana sikio la muziki. Huwa sichukii nikiambiwa wimbo ni mbaya lakini machozi huwa yananitoka kwa sababu mimi naamini nimetengeneza hit alafu mtu anakwambia hamna kitu. Hata huu wimbo wa unanimaliza ndio ulipita kati ya nyimbo tano nilizotengeneza na nyingine zilizobaki wamenishauri nisiziweke kwenye albam"- Ray C alifunguka.

Aidha Ray C amewataka wasanii wengine kutojiamini kupitiliza kiasi cha kuchukua wimbo studio na kuupeleka kwa mashabiki pasipokupata ushauri kwani kufanya hivyo ndicho chanzo cha nyimbo kupoteza ladha mapema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.