Nitajiuzulu kwa uamuzi wa wananchi: Maalim Seif - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nitajiuzulu kwa uamuzi wa wananchi: Maalim Seif

Dar  es Salaam. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif  amesema yuko tayari kujizulu siasa na kuwapisha wengine iwapo wananchi watamwomba kufanya hivyo.

Maalim Seif ambaye yuko katika ziara isiyo rasmi jijini Dar es salaam amesema hayo leo (Jumatano) katika mahojiano kwenye kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds tv kila siku za wiki.

Amesema anaamini katika siasa za mshikamano unaoundwa na wananchi hivyo iwapo wananchi hao wataona muda wake wa kutumika kwenye siasa unatosha basi atatii ridhaa yao na kujiweka kando.

“Suala la kujiuzulu siyo jambo la ajabu…mimi najua napendwa na wananchi tena napendwa kweli. Jambo moja kuwa iwapo wakisema sasa inatosha niondoke nitafanya hivyo,” amesema Maalim Seif.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.