"Niliamini sitamuona tena Roma" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

"Niliamini sitamuona tena Roma"

Nancy Mshana mke wa Roma amefunguka na kusema alikata tamaa juu ya mume wake, ambaye alitekwa na kupotea kwa siku kadhaa bila kufahamika alipokuwa licha ya jitihada zilizokuwa zikifanyika na watu wake wa karibu na vyombo vya usalama bila mafanikio.

Nancy Mshana akimlisha keki mume wake Roma Mkatoliki, katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Nancy alisema hayo katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na kudai hakutegemea tena kama angekuwa na mume wake huyo katika siku hiyo ila anashukuru kwa uwezo wake Mungu ambaye alitenda miujiza na kufanya mume wake kupatikana. 

"Ilifika wakati nilikata tamaa na kuamini kuwa sitakuwa na wewe katika sikukuu ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ya mwaka huu!! Lakini Mungu Baba wa Mbinguni akasema 'NO'" alisema Nancy 

Mbali na hilo rapa Roma Mkatoliki ambaye sasa anaendelea vyema na hali yake kuzidi kuimarika zaidi kufuatia majeraha aliyopata wakati alipotekwa, anasema ameamua sasa kuendelea na maisha yake ya muziki kama kawaida hivyo mashabiki wasishangae kumuona stejini muda wowote kuanzia sasa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.