Neymar kupanda kizimbani kujibu mashtaka ya ulaghai - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Neymar kupanda kizimbani kujibu mashtaka ya ulaghai

Jaji mmoja katika jiji la Madrid ameamuru mchezaji nyota wa Brazil Neymar afikishwe kizimbani kujibu mashtaka kuhusu ulaghai na ulaji rushwa alipokuwa anahamia Barcelona mwaka 2013.

Wazazi wa Neymar pamoja na rais wa klabu ya Barcelona wa wakati huo Josep Maria Bartomeu na mrithi wake Sandro Roselli pia wametajwa miongoni mwa washtakiwa.

Klabu ya Barca pamoja na Santos ya Brazil, alikotoka Neymar pia zinatakwia kortini.

Waendeshaji mashtaka wanadai klabu zote mbili zilidunisha makadirio ya thamani halisi yamchezaji huyo ili kulaghai kampuni ya Brazil ambayo ingefaidi kutokana na uhamisho wake.
Kesi hiyo itasikizwa mjini Madrid.

Neymar ametakiwa kuweka dhamana ya zaidi ya dola milioni tatu unusu.

Kesi hiyo itokana na malalamiko kutoka kwa kundi la uwekezaji la Brazil DIS, ambalo lilimiliki asilimia 40 ya haki za uhamisho wa Neymar.

Kundi hilo linadai kupokea pesa kidogo kinyume na matarajio yao wakati Neymar alipojiunga na Barca kutoka Santos kwa kitita cha pauni milioni 49 mwaka 2013.

''Klabu ya Santos FC, mamake Neymar Nadine Goncalves, na kampuni ya familia ya N&N inayomilikiwa na wazazi wa mchezaji huyo mweye umri wa miaka 25 pia watakabiliwa na mashtaka ya ufisadi na kutumia udanganyifu,'' mahakama kuu ya Uhispania ilisema Februari mwaka huu.

Waendesha mashtaka wanataka mchezaji huyo kufungwa kwa miaka miwili na kutozwa faini ya karibu pauni milioni 8 .

Hata kama mchezaji huyo wa kimataifa atapatikana na hatia, itakuwa vigumu kwake kufugwa jela.

Chini ya mfumo wa sheria ya Uhispinia, kifungo cha chini ya miaka miwili kwa kawaida hutupiliwa mbali.

Waendesha mashtaka pia wanataka kuwatoza faini £7.2m kwa Barcelona na £5.6m kwa klabu ya Santos.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.