Mourinho amkejeli Wenger - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mourinho amkejeli Wenger

Mourinho amempiga kijembe mpinzani wake Arsene Wenger walau amepata kitu cha kuzungumza na kuwapa furaha mashabiki wake baada ya Arsenal kuichapa Manchester United 2-0 juzi Jumapili kwenye Ligi Kuu England.

Mabao ya kipindi cha pili yalifungwa na Granit Xhaka na staa wa zamani wa Man United, Danny Welbeck walitosha kumpa Wenger ushindi wake wa kwanza mbele ya Mourinho kwenye Ligi Kuu England baada ya kukutana mara 13. Kabla ya mechi, Mourinho alitangaza amani dhidi ya Wenger, lakini amebadilika na kuonyesha wazi kwamba wawili hao hawawezi kuwa kitu kimoja hata siku moja.

"Mashabiki wa Arsenal wamefurahi na mimi nimefurahi kwa ajili yao," alisema Mourinho, ambaye timu yake ilikuwa haijapoteza kwenye ligi kwa mechi 25.

"Hii ni mara ya kwanza kuja kwao ama Highbury au Emirates kisha wakafurahi. Niliondoka Highbury wakiwa wanalia. Niliondoka Emirates wakiwa wanalia. Walikuwa wakitembea mitaani vichwa chini. Hatimaye wameweza kuimba na kupeperusha skafu zao. Safi sana.

"Wao ni klabu kubwa. Unadhani naweza kufurahia kuwa kwenye klabu kubwa kama Arsenal kisha haibebi mataji? Siwezi kufurahia hilo. Arsene Wenger si kocha mdogo, ni kocha mkubwa, hivyo kuwa na rekodi ya kushinda mechi nyingi dhidi yake si jambo dogo. Kawaida ni kushinda, kupoteza na kutoa sare, lakini kabla ya hapo haikuwa kawaida.

"Kwangu mimi sijali, sina tatizo, tulipeana mikono kabla ya mechi na tulipeana mikono baada ya mechi. Wakati wa mechi sikupendezwa na kile kile ambacho siku zote sipendezwi nacho, alikuwa akimpa presha sana mwamuzi wa akiba moja wote."

Kisha Mourinho akampiga kijembe Wenger kwa kudai kwamba alicheza mechi hiyo kwa kujilinda baada ya kuweka ukuta wa mabeki watano.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.