Mkude awapania Mbao FC - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mkude awapania Mbao FC

NAHODHA WA KLABU YA SIMBA, JONAS MKUDE.

NAHODHA wa klabu ya Simba, Jonas Mkude, amesema licha ya kutambua ugumu wa mchezo wao wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC, hawana namna zaidi ya kuhakikisha wanapata ushindi ili kushiriki michuano ya kimataifa.

Tumaini pekee la klabu hiyo katika kushiriki michuano ya kimataifa mwakani ni kutwaa ubingwa wa kombe hilo la FA baada ya kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Akizungumza na Nipashe jana, Mkude alisema uwezekano wa wao kutwaa ubingwa msimu huu ni mgumu kwa kuwa njia pekee ya kufanya hivyo ni kuhakikisha Yanga wanaoongoza ligi wanapoteze michezo yao [wa jana dhidi ya Toto Africans na ujao dhidi ya Mbao FC] na Simba ishinde mchezo wake wa mwisho.

"Nina uhakika Simba itashiriki mashindano ya kimataifa mwakani japo pia lengo na dhamira yetu ilikuwa kutwaa ubingwa msimu huu," alisema Mkude.

Yanga waliopo kileleni mwa ligi hiyo, jana walicheza mchezo wao mmoja wa kiporo dhidi ya Toto Africans na ushindi ulitegemewa kuwafanya waongoze ligi kwa tofauti ya pointi tatu na kunogesha sherehe zao za ubingwa.

Simba pamoja na timu nyingine za Ligi Kuu Bara, zitacheza michezo yao ya mwisho ya ligi msimu huu Jumapili ijayo.

Kikosi hicho cha kocha Joseph Omog, kitacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Mwadui FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.