Miaka saba jela kwa kuiba kichanga - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Miaka saba jela kwa kuiba kichanga

Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imemhukumu   kifungo cha miaka saba, Happness Mwakisyala (28) mkazi wa Majengo, Tunduma baada ya kukiri kosa la kutaka kumuiba mtoto  mchanga wa umri wa saa 12 kwenye hospitali ya wilaya hiyo.

Hakimu wa Mahakama hiyo, Nemes Chami amesema baada ya mshtakiwa huyo kukiri mwenyewe kosa hilo, mahakama ilijidhirisha maelezo yake hivyo kumhukumu kifungo cha miaka saba gerezani ili iwe fundisho kwa wengine kwani vitendo hivyo vimeanza kushamiri katika jamii wilayani hapo.

“Mahakama haioni sababu ya kuchukua muda mrefu katika shauri hili, kwa sababu mshtakiwa mwenyewe amekiri kosa lake, na mahakama imejiridhisha  maelezo yake na yaliyotolewa upande wa Jamhuri, hivyo inamtia hatiani mshtakiwa huyo na atakwenda jela miaka saba,”amesema.

Awali mwendesha mashtaka, Samwel Siro aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kutokana na vitendo vya kuiba watoto kukithiri hivi sasa katika jamii   ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia kama hiyo.

Mshtakiwa huyo alidaiwa kutenda kosa hilo saa 11 alfajiri ya  Mei 11, mwaka huu ambapo kwa makusudi aliingia kwenye wodi  ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi   na kumuiba mtoto wa kiume kisha kwenda kumficha chooni kabla ya kuondoka naye.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.