Mavugo atamba makali ya Simba kuhamia Bara - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mavugo atamba makali ya Simba kuhamia Bara

BAADA ya timu yake kufanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya Kombe la FA , mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Burundi, Laudit Mavugo, amesema wamepanga kucheza vichapo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizobakia.

Mavugo ndiye aliyepiga krosi ya bao pekee lililofungwa na kiungo Mohammed Ibrahim katika mechi ya hatua ya nusu fainali dhidi ya Azam FC.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mavugo, alisema ushindi dhidi ya Azam umewaongezea morali wachezaji wa timu hiyo ambao bado wanaamini nafasi ya kutwaa ubingwa wa Bara bado iko wazi.

Mavugo alisema kuwa mechi dhidi ya Azam ilikuwa ngumu lakini kila mara wachezaji walikumbushana kutekeleza majukumu waliyopewa ili kuhakikisha wanafanikiwa kucheza michuano ya kimataifa mwakani.

"Tulijua ushindi katika mechi ya jana (juzi) kwetu ni muhimu zaidi, Simba inataka makombe na inataka kushiriki mashindano ya kimataifa, hatukukata tamaa licha ya kupoteza mechi za ligi pale katikati," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Polisi Rwanda.

Aliongeza kuwa kwa sasa anafuraha kuona kiwango chake kimerejea na kuisaidia Simba kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ya Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji huyo ndiye alifunga bao pekee katika mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Madini FC uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.