Mashabiki wa Arsenal wakerwa na kauli ya Arsene Wenger - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mashabiki wa Arsenal wakerwa na kauli ya Arsene Wenger

Ni wazi kwamba pamoja na ushindi wa usiku wa Jumanne lakini klabu ya Arsenal ni ngumu kumaliza katika orodha ya timu nne za juu/top four msimu huu.

Suala hili linawakera sana mashabiki wa Arsenal na wamekuwa wakipiga kelele kuhusu Wenger, karibia dunia nzima Mfaransa huyo amekuwa akipigiwa kelele.

Wengi wamekuwa hawakubaliani na kiwango cha timu yao na kumuomba Wenger awaachie timu yao na aondoke, lakini hadi sasa hakuna dalili za Wenger kuondoka.

Kibaya zaidi ni kauli aliyoitoa Mfaransa huyo kuhusu kuingia katika top four msimu huu, Wenger amewaambia mashabiki wa Arsenal kuingia top four si lolote.

Wenger anashangaa kwanini watu wanaona top four ni kitu kikubwa? “Huwezi kujua tutaishia wapi lakini swali hili nimekuwa nikilijibu sana kwamba top four sio kitu kikubwa” alisema Wenger.

Wenger anasema suala la mashabiki kujadili wao kutoingia top four linamshtua kwani sio jambo kubwa,lakini akasema watapambana kuingia katika top four lakini hata wakishindwa sio jambo kubwa.

Arsenal wana alama 72 huku Liverpool aliyeko nafasi ya 4 akiwa na alama 73 na hii inamaanisha kwamba Liverpool wakishinda katika mchezo wao wa mwisho itawafanya Arsenal kumaliza nafasi ya 5

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.