Manecky Aeleza Uwezekano wa Kufanya Kazi Tena na Diamond - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Manecky Aeleza Uwezekano wa Kufanya Kazi Tena na Diamond

Prodyuza kutoka AM Records, Manecky amesema yeye kufanya tena kazi na diamand Platnumz kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma itategemea zaidi mipango ya management ya msanii huyo.

Manecky ambaye alitengeneza hit za diamond kama Nataka Kulewa na Ukimuona, ameimbia show ya XXL kuwa kazi alizokwishafanya na Diamond bado zipo pengine zitakuja kutoka siku za mbeleni kama management yake itaridhia hilo.

“Project zipo ila nadhani na wao ni watu wana mipango yao lakini kuna vitu vitakuja. Kuna vitu vilitokea hapo katika unajua disappointment nyingi sana zinatokea unapodeal na wasanii, ni vitu ambavyo mara nyingi huwa vinatuumiza, mimi kama prodyuza ambaye nina experience ya miaka mingi nimeshakutana na wasanii wengi,” amesema na kuongeza.

“Kwenye project ni wao sasa, wao wana management yao, ambao wanaamua kwa kipindi hiki wafanye kipi. Kwa jinsi mimi ninavyomjua Diamond ni mtu ambaye anaweza kuwa na project za kutoa hata mpaka mwaka 2020, inawezekana hizo nyimbo tayari anazo ndani ni kuamua atoe ipi, kwa hiyo ni timing tu,” ameleza Manecky.

By Peter Akaro

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.