Malima Afikishwa Kortini, aachiwa kwa mamilioni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Malima Afikishwa Kortini, aachiwa kwa mamilioni

NAIBU waziri wa fedha wa awamu ya nne kwenye uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Adam Kighoma Ali Malima leo Mei 16, 2017 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kuwazuia polisi kufanya kazi yao.

Mlalamikaji katika kesi hiyo ni askari H.7818 PC Abdul akiwa kazini na maafisa wa Kampuni ya PBEL inayojihusisha na kukamata watu wanaopaki magari hovyo ambapo tukio hilo lilitokea jana eneo la Double Tree Hotel Masaki.

Mlalamikaji amedai alizuiliwa kutekeleza wajibu wake na waziri mstaafu huyo huku akishirikiana na wanachi kuwazuia askari hao ambapo askari huyo aliamua kupiga risasi sita hewani ili kuwatuliza watu waliokuwa wanazomea wakiongozwa na mtuhumiwa.

Hata hivyo mtuhumiwa pamoja na dereva wake walikamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Oysterbay jana na kufunguliwa kesi yenye namba OB/RB/7306/2017.

Aidha mahakama imemwachilia huru Malima kwa dhamana ya shilingi milioni tano.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.