Kutoka Arusha: Idadi ya vifo vya wanafunzi imeongezeka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kutoka Arusha: Idadi ya vifo vya wanafunzi imeongezeka

Kutoka kwenye chanzo cha kuaminika Mkoani Arusha, Mwanafunzi aliyekuwa amelazwa katika chumba cha kuhifadhia wagonjwa mahututi (ICU) Doreen Mshana amefariki leo mchana.

Kifo cha Doreen Mshana kimeongeza idadi ya vifo kufikia 36 ambapo wanafunzi ni 33, Walimu wawili na dereva mmoja baada ya ajali iliyotokea jana wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Taarifa za kifo cha binti huyo zilianza kusambaa jana kwenye mitandao ya kijamii hali iliyompelekea Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo kulitolea ufafanuzi

."Kuna mmoja walimripoti amefariki ndiyo maana wakasema 33 lakini siyo kweli waliofariki ni wanafunzi 32 walimu wawili na dereva mmoja. Hakuna kifo kilichoongezeka, taarifa zilisambaa kuwa yule mwanafunzi  aliyekuwa kapoteza fahamu amefariki lakini siyo kweli. nawataka watoa taarifa wa confirm habari kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.- alisema Mkumbo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.