Klopp: Mechi yetu ya mwisho ni kama fainali - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Klopp: Mechi yetu ya mwisho ni kama fainali

Liverpool hawatakuwa 'wajinga' kwa kudhani kwamba wataichapa kwa urahisi Middlesbrough ili kujihifadhia nafasi ya kushiriki tena katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, amesema meneja Jurgen Klopp.

The Reds wana matarajio ya kuwa miongoni mwa timu nne bora iwapo wataipiku Boro ambayo ilishushwa daraja uwanjani Anfield Jumapili katika mechi ya mwisho msimu huu.

Arsenal ambao wamo katika nafasi ya tano, wana mchezo mmoja na wamo alama nne nyuma ya Liverpool.

''Nimekuwa katika kazihii kwa miaka mingi, kutambua makosa makubwa ni kuhesabu alama kabla ya kuzipata,'' Klopp alisema baada ya ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya West Ham.

''Hatutafanya hivyo. Sentensi ya kwanza vijana wa Reds walisema katika chumba cha kubadilishia nguo kusema 'mechi moja imesalia' na sikuwa nahitajika kusema lolote. Tunataka nafasi katika ligi ya klabu Bingwa Ulaya.

Mjerumani, 49, alichukua nafasi ya Brendan Rodgers aliyepigwa kalamu mwezi Oktoba 2015, anapoelekea kuiongoza The Reds kutoka nambari nane msimu uliopita.

Kabla ya safari ya Jumapili ya kuelekea katika uwanja wa London, Liverpool ilifahamu kwamba hawatatolewa katika nafasi ya nne iwapo watashinda michezo yao miwili ya mwisho.

Hata hivyo, The Reds itajipata nafasi ya nne kabla ya mechi yao na Boro, iwapo Arsenal itashindwa kuifunga Sunderland iliyoshushwa daraja siku ya Jumanne.

"Middlesbrough hawana kitu cha kupoteza, lakini tuna kila kitu cha kupoteza,'' aliongeza meneja wa zamani wa Borussia Dortmund, Klopp.

Pia tumekuwa tukitambua ya kwamba lazima tujikaze hadi mwisho wa msimu, hilo si tatizo kwetu sisi.

Iwapo tutashinda tutastahili kuwa katika Ligi ya Mabingwa, kama sivyo, hatustahili.

"Tulipata wakati mzuri tulipokuwa tukikabiliana na West Ham, na iwapo tutapata nafasi kama hiyo kwa mchezo ujao tutakuwa na nafasi nzuri. Lakini kuhesabu alama kwa mchezo ujao ni ujinga, sisi hatufanyi hivyo.''

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.