Kagera Sugar waijia juu Simba SC - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kagera Sugar waijia juu Simba SC

Uongozi wa Kagera Sugar kupitia Meneja wake Mohammed Hussein ameitaka klabu ya Simba SC iseme ukweli kwa umma kuwa mshambuliaji Mbaraka Yussuf Abeid walimtoa kwa mkopo na wala siyo kwa mkataba wowote kama wao wenyewe wanavyodai.

Hussein amebainisha hayo baada ya Rais wa Simba SC, Evans Aveva kusema wataenda kufungua kesi mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) dhidi ya ya klabu ya klabu hiyo kwa madai ya kuwadhulumu mchezaji wao Mbaraka Yussuf waliyompeleka kwa mkopo lakini timu hiyo ikajimilikisha moja kwa moja kinyume cha sheria na makubaliano waliyowekeana.

"Simba wanatakiwa wawe wawazi na wawafahamishe watu ukweli, kwamba Mbaraka Yussuf Abeid kweli aliletwa kwetu kwa mkopo na kwa barua tu siyo kwa mkataba wowote, kwamba tulipewa barua kwamba yule mchezaji atacheza kwetu kwa mkopo". Alisema Hussein
Aidha Hussein ameedelea kubainisha baadhi ya mambo kwa kusema "Baada ya kumalizika msimu uliopita, Simba walimuhitaji Mbaraka Yussuf Abeid arejee msimbazi lakini mchezaji mwenyewe akagoma na kusema hakuwahi kusaini mkataba wowote na Wekundu hao wa msimbazi". Aliongezea Meneja huo

Pamoja na hayo Hussein amesema waliweza kufuatilia suala hilo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kujiridhisha kwamba kweli mchezaji huyo hakuwa na mkataba wowote katika kipindi hicho na kuamua kumpa wa kwao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.