Kagera Sugar nao Kupinga kadi nyekundu TFF leo Mei 10 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kagera Sugar nao Kupinga kadi nyekundu TFF leo Mei 10

TIMU ya Kagera Sugar leo inatarajiwa kuwasilisha malalamiko Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga kadi nyekundu aliyoonyeshwa mshambuliaji wao, Mbaraka Yussuf Abeid katika mchezo dhidi ya Yanga jana.

Kagera Sugar ilifungwa 2-1 na wenyeji, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na bahati mbaya mfungaji wa bao lao na mshambuliaji wao tegemeo, Mbaraka Yussuf hakumaliza mechi.

Refa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Ngole Mwangole wa Mbeya alimtoa nje kwa kadi nyekundu Mbaraka Yussuf Abeid dakika ya 87 baada ya kumchezea rafu beki wa Yanga, Kevin Yondan.

Mratibu wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein alisema kwamba wanaandikia barua TFF kupinga kadi hiyo kama ilivyo walivyowahi kufanya Yanga, kupinga kadi ya Obrey Chirwa.

Alisema mchezaji wao hakucheza rafu zaidi ya kuruka juu tu kiungwana kuwania mpira dhidi ya beki wa Yanga, Yondan. “Yondan pale alimdanganya refa, na refa akadanganyika, lakini naamini wakirudia kuangalia teknolojia ya picha za video wataona vizuri na watabatilisha maamuzi yao,”alisema. 

Alisema kadi hiyo itamkwamisha Mbaraka katika harakati zake za kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hadi sasa akiwa ana mabao 12, nyuma ya Simon Msuva wa Yanga, anayeongoza kwa mabao yake 13.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.