Jengo la Yanga kupigwa mnada - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jengo la Yanga kupigwa mnada

JENGO la makao makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es Salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.

Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa Kampuni ya Udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.

Akizungumza na gazeti hili jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwapo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.

Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la makao makuu haujafanyika.

"Ni kweli kesi iko katika Mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi," alisema kwa kifupi Mkwasa, kocha na mchezaji wa zamani wa timu hiyo.

Katika hatua nyingine, Mkwasa alisema kuwa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kinarejea jijini Dar es Salaam kati ya leo na kesho na kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

"Timu itarejea jijini katika siku mbili hizi ili kuendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiimarisha kwa lengo moja la kusaka pointi tatu muhimu katika mchezo wetu wa Jumamosi," alisema Mkwasa.

Wakati huo huo, juzi Yanga iliibamiza timu ya Buseresele ya Geita mabao 5-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa mkoani humo.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke, Anthony Matheo, Amissi Tambwe na Emmanuel Martin aliyefunga mawili.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.